Madaraka Nyerere ni Taasisi ya kielimu inayopatikana katika Shule ya Sekondari ya Nyegina, kilometa kumi na sita (16) Kusini mwa mji wa Musoma katika kijiji cha Nyegina.
Katikati ya Nyegina Sekondari /Shule ya Msingi Nyegina upande wa kaskazini kinapakana na zahanati ya Nyegina .
Kituo kinatoa fursa sawa kwa wanafunzi, wanakijiji na watu binafsi , Taasisi mbalimbali za binafsi, Serikali na wataalam wa kada zote wanaoizunguka jamii.
Kauli dhima
Elimu Kwa Maisha Bora Endelevu
MALENGO YA KITUO
1. Kuwezesha upatikanakaji wa vitabu ,machapisho na vifaa vya kufundishia kwa ajili ya wanafunzi,walimu na jamii kwa ujumla
2. Kutoa fursa kwa jamii,wanafunzi na walimu kujiendeleza kitaaluma kwa gharama nafuu
3. Kuwezesha wanafunzi, walimu na jamii kufurahia kujifunza kupitia huduma ya mtandao
4. Kusaidia upatikanaji na matumizi ya Tehama kwa jamii.
5. Kuwa kitovu cha mafunzo kwa watumishi, wakulima , wavuvi na wafugaji.
HUDUMA ZITOLEWAZO;
Kituo cha Maarifa ya Jamii na Maktaba cha Madaraka Nyerere kinatoa huduma zifuatazo; -
-Huduma za msingi za maktaba
-Mafunzo ya Komputa kwa wanafunzi, vijana na jamii nzima
-Huduma ya uchapaji, fotokopi na uandaaji wa vitabu
-Huduma za mtandao(INTANETI)
WALENGWA;
Kituo kimelenga kuhudumia
- Wanafunzi wa shule za awali
- Wanafunzi wa shule za msingi
- Wanafunzi wa sekondari
- Wanafunzi wa Elimu ya juu
- Jamii nzima inayoizunguka shule.
No comments:
Post a Comment